Tangazo la Ajira: Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 7 - SixmailizJobs

Sunday, March 1, 2026

Tangazo la Ajira: Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 7

   📢 Tangazo la Ajira: Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 7


Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

Kiwango cha Mshahara:TGS C

Idadi ya Nafasi:7

Mwisho wa Kutuma Maombi:08 Machi 2026

Namna ya Kutuma Maombi:Kupitia Ajira Portal


🗂️ Kuhusu Nafasi Hii


Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kujaza nafasi saba (7) za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary Grade II).


Hii ni nafasi muhimu katika kuhakikisha shughuli za ofisi zinaendeshwa kwa ufanisi, nidhamu na weledi wa hali ya juu.


✅ Majukumu Makuu


Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri

- Kupokea wageni na kuwaelekeza ipasavyo

-Kutunza kumbukumbu za miadi, vikao, safari na ratiba za kazi

-Kutafuta, kupokea na kusambaza majalada na nyaraka

-Kuandaa maandalizi ya vikao na dondoo muhimu

-Kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi

-Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa kazi


🎓 Sifa za Mwombaji


Mwombaji anatakiwa kuwa na:


(i).Elimu ya Kidato cha Nne au Sita.


(ii). Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili (Secretarial Studies).


(iii). Ufaulu wa Hatimkato (Shorthand) ya Kiswahili na Kiingereza angalau maneno 80 kwa dakika.


(iv).Ujuzi wa programu za kompyuta: **Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.


(v).Mafunzo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.


🌟 Ushauri Muhimu wa Jinsi ya Kushinda Kwenye Ushindani Mkubwa


•Kwa kuwa nafasi ni 7 tu na waombaji ni wengi, zingatia yafuatayo:


1️⃣ Hakikisha Taarifa Zako Zimekamilika


-Jaza taarifa zako zote kwa usahihi kwenye Ajira Portal.

-Pakia vyeti vilivyothibitishwa na visivyo na makosa ya majina.


 2️⃣ Andaa CV Inayovutia


-Onyesha uzoefu wowote wa ofisi hata kama ni wa kujitolea (volunteer).


-Taja kasi yako ya uchapaji (typing speed) kama ni kubwa kuliko 80 w.p.m


3️⃣ Jiandae kwa Usaili Mapema


-Fanya mazoezi ya kuchapa kwa muda (timed typing)


-Rudia maswali ya msingi ya maadili ya kazi za ofisi


-Jifunze namna ya kujieleza kwa kujiamini na kwa nidhamu


4️⃣ Onyesha Tofauti Yako


Waajiri hutafuta mtu:


-Mwenye nidhamu na muonekano wa kitaalamu


-Anayejua kuhifadhi siri za ofisi


-Mwenye mawasiliano mazuri kwa mdomo na maandishi


💬 Maoni Yetu


Nafasi hii ni nzuri kwa wahitimu wa Uhazili wanaotaka kuingia au kukuza taaluma yao Serikalini. Ikiwa una sifa zilizotajwa, usisite kutuma maombi mapema kabla ya tarehe ya mwisho.


Kumbuka:


> Mafanikio si bahati — ni maandalizi sahihi yanapokutana na fursa.


🔥Kuwa smart and focused utakuwa the Best bila Kukata tamaa


🔔 Je, una swali au unahitaji mwongozo wa jinsi ya kutuma maombi kupitia Ajira Portal?

Acha maoni yako hapa chini;

 👉Tutakujibu Haraka, Tupo Karibu yako na Pamoja na wewe kila hatua unayopiga.


#AjiraMpya #Serikali #OfficeManagement #Tandahimba #AjiraPortal

1 comment:

Translate